
Video Mpya ya Utangulizi wa Kozi: Je, Mungu hutimiza ahadi zake? (Kiarabu chenye Maandishi ya Kiingereza)
Akamtoa nje, akamwambia, “Tazama juu mbinguni, uzihesabu nyota, kama unaweza kuzihesabu.” Kisha akamwambia, “Hivyo ndivyo wazao wako watakavyokuwa.” – Mwanzo 15:5
Utangulizi
Kusudi la kozi hii ni kutoa muhtasari wa Biblia.
Bwana Yesu mwenyewe alitupa ufunguo aliposema: “ Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele, maandiko haya ndiyo yanayonishuhudia mimi. Lakini mnakataa kuja kwangu ili mpate uzima.”( Yohana 5:39-40).
Akawaambia, “Haya ndiyo yale niliyowaambia nilipokuwa bado Pamoja nanyi, kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika Sheria ya Musa, Manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.” Luka 24: 44-45).
Alipozungumza juu ya ‘Sheria ya Musa, manabii na Zaburi’ Yesu alikuwa akimaanisha Agano lote la Kale, kwa sababu, katika siku zake, watu wa Kiyahudi waligawanya Agano la kale katika sehemu tatu.
Yesu alikuja kutimiza Agano la Kale na mara kwa mara aliitaja kuwa mamlaka nyuma ya mafundisho yake.
Hivyo, mada kuu ya Bibilia nzima ni mpango wa Mungu kutuma Mwokozi, ambaye ni Bwana Yesu Kristo.
Malengo ya Kozi 101
- Kuona hadithi ya umoja ya ukombozi wa Mungu kupitia Yesu.
- Ilikuelewa jinsi ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu ilitimilia katika Kristo.
- Kuongeza Imani katika uaminifu wa Mungu kwa Neno lake na baraka zake kwa wale wanaomwamini Kristo kwa wokovu wao.
- Kuhamasishwa kushiriki katika utimilifu unaoendelea wa mpango wa Mungu wa baraka kwa kuleta ujumbe wa injili kwa watu wote.
Masomo
| ❶ | Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu: Baraka kwa watu wote |
| ❷ | Mchoro wa Historia ya Agano la Kale |
| ❸ | Injili: Maelezo ya shahidi wa Macho kuhusu ujio wa masihi Kristo |
| ❹ | Metendo na kanisa la awali: Kuhubiri Imani katika Yesu Masihi hadi mwisho wa dunia |
| ❺ | Nyaraka : Kufundisha kwa Kanisa |
Kwa kupakua, kutumia, na/au kuwa na nyenzo za Kuendendelea Pamoja unakubali kutobadilisha nyenzo zetu na kuziwakilisha kama zako au kujaribu kuziuza kwa njia yoyote ile.
* Kumbuka: Sio programu zote za PDF zitaonyesha sehemu zinazoweza kuandikwa. Ikiwa una matatizo, tafadhali jaribu Adobe Acrobat Reader kutazama/kujaza faili ya PDF ya kozi.
