
Video ya Utangulizi ya Kozi Mpya: Je, Mungu ni Baba yangu? (Kiarabu chenye Manukuu ya Kiingereza)
Mungu akaona kila kitu alichokifanya kuwa ni chema kabisa.
Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyokamilika pamoja na vitu vyote vilivyomo. Siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyofanya; siku hiyo ya saba Mungu akapumzika baada ya kazi yake yote aliyofanya.
Mwanzo 1:31a na 2:1-2
Ujumbe wa Injili ni habari njema kwa wanadamu wote. Inategemea neema — sio kustahili — na inasimama kinyume na dini zilizotengenezwa na wanadamu.
- Dini zinasema:
“Fanya! Fanya hivi, fanya hivyo, na tunatumai utastahili wokovu wa Mungu.”
- Wokovu wa kweli uliofunuliwa kutoka mbinguni unasema:
“Imekamilika! Yesu tayari amelipa gharama kamili ya wokovu wetu.”
Ujumbe huu mwanzoni unaweza kuonekana kuwa wa kipumbavu na hata usio wa haki kwa watu wengi. Hata hivyo kweli za msingi za Injili zimewekwa kutoka katika sura za kwanza za Mwanzo na kuelezwa na kukuzwa katika Biblia nzima.
Mfululizo huu wa masomo unatokana na sura hizi tatu za kwanza za Biblia. Marejeleo kutoka sehemu nyingine za Biblia kwa kulinganisha na kujifunza zaidi yanatolewa inavyofaa.
Kila somo linatoa ukweli muhimu wa Habari Njema za wokovu kutoka kwa dhambi na hukumu hadi uhusiano uliorejeshwa na Mungu kupitia Yesu Kristo. Madhumuni ya kozi hii ni kuwezesha kila mshiriki kuelewa kikamilifu na kueleza kwa ujasiri kwa wengine ujumbe wa kipekee na wa ajabu wa Injili.
Vifungu vya Biblia vya kujifunza kwa moyo ni: Waefeso 2:4-5 na Yohana 1:29.
Masomo
❶ Kuna Mungu mmoja, Muumba wetu.
❷ Mwanadamu, pamoja na uumbaji wote wamepotoshwa na dhambi.
❸ Mungu ametoa njia ya wokovu.
❹ Yesu Kristo ndiye Mwokozi wetu.
❺ Kristo atarudi duniani kukamilisha wokovu wetu.
Updated October 2024
Kwa kupakua, kutumia, na/au kuwa na nyenzo za Kuendendelea Pamoja unakubali kutobadilisha nyenzo zetu na kuziwakilisha kama zako au kujaribu kuziuza kwa njia yoyote ile.
* Kumbuka: Sio programu zote za PDF zitaonyesha sehemu zinazoweza kuandikwa. Ikiwa una matatizo, tafadhali jaribu Adobe Acrobat Reader kutazama/kujaza faili ya PDF ya kozi.
